Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Methali 5:16 - Swahili Revised Union Version Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Biblia Habari Njema - BHND Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Neno: Bibilia Takatifu Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? Neno: Maandiko Matakatifu Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? BIBLIA KISWAHILI Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? |
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
Bustani iliyofungwa ni dada yangu, bibi arusi, Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa mhuri.
Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi.
Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani; Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao; Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.
Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande.
Alikuwa na watoto thelathini wa kiume; na binti thelathini aliwaoza nje ya ukoo wake, kisha akaleta wanawake thelathini kutoka mahali pengine kwa ajili ya hao wanawe. Akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka saba.