Methali 4:19 - Swahili Revised Union Version Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae. Biblia Habari Njema - BHND Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae. Neno: Bibilia Takatifu Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae. BIBLIA KISWAHILI Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho. |
Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watateremshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema BWANA.
Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;