Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Methali 30:5 - Swahili Revised Union Version Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maneno yote ya Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia. Biblia Habari Njema - BHND Maneno yote ya Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maneno yote ya Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia. Neno: Bibilia Takatifu “Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. Neno: Maandiko Matakatifu “Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. BIBLIA KISWAHILI Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio. |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Mwamba wangu na ngome yangu, Nguzo yangu na mwokozi wangu Ngao yangu ninayemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.