Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 22:31 - Swahili Revised Union Version

31 Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Mwenyezi Mungu halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

31 Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 22:31
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na kimbilio langu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.


nawe ukauona moyo wake kuwa mwaminifu mbele zako, ukafanya agano naye, kumpa nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Myebusi, na Mgirgashi, naam, kuwapa wazao wake; nawe umetimiza ahadi yako kwani u mwenye haki.


Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu; Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; Wala Mwenyezi kufanya uovu.


Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.


Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.


BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote.


Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.


Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.


Uishike ngao na kikingio, Uinuke unisaidie.


Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi


Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.


Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.


Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.


Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;


Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo