Methali 30:22 - Swahili Revised Union Version Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtumwa anayekuwa mfalme; mpumbavu anayeshiba chakula; Biblia Habari Njema - BHND Mtumwa anayekuwa mfalme; mpumbavu anayeshiba chakula; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mtumwa anayekuwa mfalme; mpumbavu anayeshiba chakula; Neno: Bibilia Takatifu mtumwa anapokuwa mfalme, mpumbavu anaposhiba chakula, Neno: Maandiko Matakatifu Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula, BIBLIA KISWAHILI Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; |
Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa tajiri sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.
Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.
Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa mkosa adabu na mwovu; naye alikuwa wa ukoo wa Kalebu.
Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.