Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao.
Methali 30:2 - Swahili Revised Union Version Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi ni mpumbavu mno, wala si mtu; nayo akili ya binadamu sina. Biblia Habari Njema - BHND Mimi ni mpumbavu mno, wala si mtu; nayo akili ya binadamu sina. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi ni mpumbavu mno, wala si mtu; nayo akili ya binadamu sina. Neno: Bibilia Takatifu “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. Neno: Maandiko Matakatifu “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. BIBLIA KISWAHILI Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu; |
Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao.
Maneno ya Aguri mwana wa Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.
Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.