Methali 3:25 - Swahili Revised Union Version Usiogope hofu ya ghafla, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu, Biblia Habari Njema - BHND Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu, Neno: Bibilia Takatifu Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, Neno: Maandiko Matakatifu Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, BIBLIA KISWAHILI Usiogope hofu ya ghafla, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. |
Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.
Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi.
Nami nitapiga kambi yangu pande zote za nyumba yangu ili kuwapinga adui, mtu awaye yote asipite ndani yake wala kurudi; wala mtu aoneaye hatapita tena kati yao; kwa maana sasa nimeona kwa macho yangu.
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.
Lakini hata mkiteswa kwa sababu ya kutenda haki, mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.