Methali 28:5 - Swahili Revised Union Version Watu waovu hawaelewi na haki; Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Wapotovu hawaelewi haki, bali wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu wanaielewa kikamilifu. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao bwana wanaielewa kikamilifu. BIBLIA KISWAHILI Watu waovu hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote. |
Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.
Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.
Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.
Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.