Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Methali 26:5 - Swahili Revised Union Version Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Biblia Habari Njema - BHND Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Neno: Bibilia Takatifu Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. |
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;