Methali 25:11 - Swahili Revised Union Version Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha. Biblia Habari Njema - BHND Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha. Neno: Bibilia Takatifu Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. Neno: Maandiko Matakatifu Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. BIBLIA KISWAHILI Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. |
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Huyo Mhubiri akachunguza ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.
Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.