BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.
Methali 24:9 - Swahili Revised Union Version Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Biblia Habari Njema - BHND Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Neno: Bibilia Takatifu Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. Neno: Maandiko Matakatifu Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. BIBLIA KISWAHILI Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. |
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.
BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;