Methali 23:9 - Swahili Revised Union Version Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiseme maneno yako mbele ya mpumbavu, maana atapuuza hekima ya maneno yako. Biblia Habari Njema - BHND Usiseme maneno yako mbele ya mpumbavu, maana atapuuza hekima ya maneno yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiseme maneno yako mbele ya mpumbavu, maana atapuuza hekima ya maneno yako. Neno: Bibilia Takatifu Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako. Neno: Maandiko Matakatifu Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako. BIBLIA KISWAHILI Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako. |
Lakini watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana ilikuwa amri ya mfalme, kwamba, Msimjibu neno.
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?
Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena kuhusu habari hiyo.