Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
Methali 23:7 - Swahili Revised Union Version Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana moyoni mwake anahesabu unachokula. Atakuambia, “Kula, kunywa!” Lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe. Biblia Habari Njema - BHND maana moyoni mwake anahesabu unachokula. Atakuambia, “Kula, kunywa!” Lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana moyoni mwake anahesabu unachokula. Atakuambia, “Kula, kunywa!” lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri kuhusu gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. BIBLIA KISWAHILI Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. |
Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
Na katika habari za wafalme hao wawili, mioyo yao watanuia kutenda madhara, nao watasema uongo walipo pamoja mezani; lakini hilo halitafanikiwa; maana mwisho utatokea wakati ulioamriwa.
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.