Methali 22:17 - Swahili Revised Union Version Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Biblia Habari Njema - BHND Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Neno: Bibilia Takatifu Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, Neno: Maandiko Matakatifu Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, BIBLIA KISWAHILI Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; |
Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.
Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu.
Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku);
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.