Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami.
Methali 22:12 - Swahili Revised Union Version Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu. Neno: Bibilia Takatifu Macho ya Mwenyezi Mungu hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. Neno: Maandiko Matakatifu Macho ya bwana hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. BIBLIA KISWAHILI Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. |
Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami.
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga.
lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;