Ni nani atambuaye maovu yetu? Tumepanga njama kwa werevu mwingi, Maana katika moyo wa mtu na fikira mengi yamefichika.
Methali 20:5 - Swahili Revised Union Version Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo. Biblia Habari Njema - BHND Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo. Neno: Bibilia Takatifu Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. Neno: Maandiko Matakatifu Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. BIBLIA KISWAHILI Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. |
Ni nani atambuaye maovu yetu? Tumepanga njama kwa werevu mwingi, Maana katika moyo wa mtu na fikira mengi yamefichika.
Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.