Methali 20:30 - Swahili Revised Union Version Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikia ndani ya mtima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mapigo yanayoumiza ni dawa ya kuondoa uovu; viboko husafisha nafsi mpaka ndani kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Mapigo yanayoumiza ni dawa ya kuondoa uovu; viboko husafisha nafsi mpaka ndani kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mapigo yanayoumiza ni dawa ya kuondoa uovu; viboko husafisha nafsi mpaka ndani kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Mapigo na majeraha huusafisha ubaya, nayo michapo hutakasa utu wa ndani. Neno: Maandiko Matakatifu Mapigo na majeraha huusafisha ubaya, nayo michapo hutakasa utu wa ndani. BIBLIA KISWAHILI Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikia ndani ya mtima. |
Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara; Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.