Methali 2:9 - Swahili Revised Union Version Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Biblia Habari Njema - BHND Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki, na sawa: yaani kila njia nzuri. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki na sawa: yaani kila njia nzuri. BIBLIA KISWAHILI Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. |
Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.