Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji.
Methali 2:4 - Swahili Revised Union Version Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; Biblia Habari Njema - BHND ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; Neno: Bibilia Takatifu na ukiitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, Neno: Maandiko Matakatifu na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, BIBLIA KISWAHILI Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; |
Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji.
Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia kuliko watafutavyo hazina iliyostirika;
Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Yule bwana akamsifu wakili asiyemwaminifu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru.