Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.
Methali 16:9 - Swahili Revised Union Version Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Biblia Habari Njema - BHND Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Mwenyezi Mungu huelekeza hatua zake. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali bwana huelekeza hatua zake. BIBLIA KISWAHILI Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. |
Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.
nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.
Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikia.