Methali 14:18 - Swahili Revised Union Version Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa. Biblia Habari Njema - BHND Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa. Neno: Bibilia Takatifu Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. Neno: Maandiko Matakatifu Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. BIBLIA KISWAHILI Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa. |
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;