Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 14:19 - Swahili Revised Union Version

19 Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Waovu watapiga magoti mbele ya watu wema, watu wabaya mlangoni mwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Waovu watapiga magoti mbele ya watu wema, watu wabaya mlangoni mwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Waovu watapiga magoti mbele ya watu wema, watu wabaya mlangoni mwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Wapotovu watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.

Tazama sura Nakili




Methali 14:19
17 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.


Wakasema, Mtumishi wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.


Yehoshafati akasema, Neno la BWANA analo huyu. Basi mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia.


Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.


Tena hao watumishi wako wote wataniteremkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.


Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni BWANA, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee BWANA dhabihu.


Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.


Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa.


Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.


Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.


Wakaja wakawasihi; na walipokwisha kuwatoa nje, wakawaomba watoke katika mji ule.


Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali nitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo