Methali 1:21 - Swahili Revised Union Version Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema huita juu ya kuta, hutangaza penye malango ya mji: Biblia Habari Njema - BHND huita juu ya kuta, hutangaza penye malango ya mji: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza huita juu ya kuta, hutangaza penye malango ya mji: Neno: Bibilia Takatifu kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: Neno: Maandiko Matakatifu kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: BIBLIA KISWAHILI Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. |
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.