Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Methali 1:15 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe mwanangu usiandamane nao, uzuie mguu wako usifuatane nao. Biblia Habari Njema - BHND Wewe mwanangu usiandamane nao, uzuie mguu wako usifuatane nao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe mwanangu usiandamane nao, uzuie mguu wako usifuatane nao. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. |
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
BWANA awaambia watu hawa hivi, Hivyo ndivyo walivyopenda kutangatanga; hawakuizuia miguu yao; basi, BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, atawapatiliza dhambi zao.
Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.