Na yeyote atakayelaani jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzaliwa, hapo atakapolaani jina la BWANA atauawa.
Mathayo 9:3 - Swahili Revised Union Version Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” Biblia Habari Njema - BHND Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” Neno: Bibilia Takatifu Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” BIBLIA KISWAHILI Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. |
Na yeyote atakayelaani jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzaliwa, hapo atakapolaani jina la BWANA atauawa.
Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.
Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
Basi, wale Waandishi na Mafarisayo wakaanza kuulizana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?