Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Mathayo 9:26 - Swahili Revised Union Version Habari hizi zikaenea katika nchi ile yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote. Biblia Habari Njema - BHND Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote. Neno: Bibilia Takatifu Habari hizi zikaenea katika maeneo yale yote. Neno: Maandiko Matakatifu Habari hizi zikaenea katika maeneo yale yote. BIBLIA KISWAHILI Habari hizi zikaenea katika nchi ile yote. |
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.
Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa limeenea, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake.
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaendea Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.
Kwa maana mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.