Mathayo 7:29 - Swahili Revised Union Version kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka. Biblia Habari Njema - BHND Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka. Neno: Bibilia Takatifu kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria. Neno: Maandiko Matakatifu kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria. BIBLIA KISWAHILI kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao. |
Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.