Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Mathayo 27:12 - Swahili Revised Union Version Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno. Biblia Habari Njema - BHND Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno. Neno: Bibilia Takatifu Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. BIBLIA KISWAHILI Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno. |
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.