Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.
Mathayo 26:46 - Swahili Revised Union Version Ondokeni, twende zetu! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amkeni; twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.” Biblia Habari Njema - BHND Amkeni; twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amkeni; twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.” Neno: Bibilia Takatifu Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” Neno: Maandiko Matakatifu Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” BIBLIA KISWAHILI Ondokeni, twende zetu! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia. |
Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.
Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliuelekeza uso wake kwenda Yerusalemu;
Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.
Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.