Mathayo 25:5 - Swahili Revised Union Version Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala. Biblia Habari Njema - BHND Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala. Neno: Bibilia Takatifu Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala. Neno: Maandiko Matakatifu Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala. BIBLIA KISWAHILI Hata bwana harusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. |
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;
Nawaambia, atawapatia haki upesi; lakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akakondisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.