Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mathayo 20:13 - Swahili Revised Union Version

Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana nami mshahara wa dinari moja?

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana nami mshahara wa dinari moja?

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana nami mshahara wa dinari moja?

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja?

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja?

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mathayo 20:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako, Au je! Wasema, Ni haki yangu mbele za Mungu,

Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?

Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

Naye alipokwisha kupatana na wafanya kazi kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.

Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.

La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwa nini umeniumba hivi?