Mathayo 18:11 - Swahili Revised Union Version Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.] Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea.] (Taz Luka 19:10). Biblia Habari Njema - BHND Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea.] (Taz Luka 19:10). Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichopotea.] Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichopotea.] BIBLIA KISWAHILI Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.] |
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisini na tisa, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
Bali ilibidi kusherehekea na kushangilia kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.
Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.