Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Mathayo 17:11 - Swahili Revised Union Version Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawajibu, “Kweli, Elia atakuja kutayarisha mambo yote. Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawajibu, “Kweli, Elia atakuja kutayarisha mambo yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawajibu, “Kweli, Elia atakuja kutayarisha mambo yote. Neno: Bibilia Takatifu Isa akawajibu, “Ni kweli, Ilya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawajibu, “Ni kweli, Ilya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. BIBLIA KISWAHILI Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, |
Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?
ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.