lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
Mathayo 14:10 - Swahili Revised Union Version akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo akaagiza Yahya akatwe kichwa mle gerezani. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo akaagiza Yahya akatwe kichwa mle gerezani. BIBLIA KISWAHILI akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. |
lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
Nimewapiga watoto wako bure; hawakukubali kurudiwa; upanga wenu wenyewe umewala manabii wako, kama simba aharibuye.
Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi karamuni pamoja naye, akaamuru apewe;
ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.
Lakini Herode akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.
Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.