Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Mathayo 10:30 - Swahili Revised Union Version lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Biblia Habari Njema - BHND Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Neno: Bibilia Takatifu Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. BIBLIA KISWAHILI lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. |
Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Sulemani Akasema, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele wake mmoja hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.
Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko Shomoro wengi.
Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea.
Lakini watu wakamwambia Sauli, Je! Atakufa Yonathani, ambaye ndiye aliyeufanya huo wokovu mkuu katika Israeli? Hasha! Kama aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa kichwa chake; kwa maana ametenda kazi pamoja na Mungu leo. Hivyo hao watu wakamponya Yonathani, asife.