Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 14:11 - Swahili Revised Union Version

11 Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Yule mwanamke akamwambia, “Tafadhali, mfalme, niombee kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi cha mauaji ya mwanangu asifanye hatia nyingine kubwa ya kumwua yule mtoto wangu mwingine.” Mfalme Daudi akamwambia, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Yule mwanamke akamwambia, “Tafadhali, mfalme, niombee kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi cha mauaji ya mwanangu asifanye hatia nyingine kubwa ya kumwua yule mtoto wangu mwingine.” Mfalme Daudi akamwambia, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Huyo mwanamke akasema, “Basi mfalme na amwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wake, ili kuzuia mlipiza kisasi cha damu kuongeza juu ya uharibifu, ili mwanangu asije akaangamizwa.” Mfalme akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, hakuna unywele mmoja wa kichwa cha mwanao utakaoanguka chini.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Huyo mwanamke akasema, “Basi mfalme na amwombe bwana Mwenyezi Mungu wake ili kuzuia mlipiza kisasi cha damu kuongeza juu ya uharibifu, ili kwamba mwanangu asije akaangamizwa.” Mfalme akasema, “Hakika kama aishivyo bwana, hakuna unywele mmoja wa kichwa cha mwanao utakaoanguka chini.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 14:11
18 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,

Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe.

Mfalme akasema, Yeyote atakaye kuambia neno, mlete kwangu, naye hatakugusa tena.

Mwanamke akasema, Mwache mjakazi wako, nakusihi, niseme neno moja kwa bwana wangu mfalme. Akasema, Haya nena.

Basi mfalme akamwambia Yoabu, Angalia sasa, nimekata shauri hili; nenda, ukamrudishe tena yule kijana Absalomu.

Sulemani Akasema, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele wake mmoja hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.

nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.

Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua.

au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye.

na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwona, naye yuko nje ya mpaka wa mji wake wa makimbilio, na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwua huyo mwuaji, hatakuwa na hatia ya damu;

lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.

Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea.

Lakini watu wakamwambia Sauli, Je! Atakufa Yonathani, ambaye ndiye aliyeufanya huo wokovu mkuu katika Israeli? Hasha! Kama aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa kichwa chake; kwa maana ametenda kazi pamoja na Mungu leo. Hivyo hao watu wakamponya Yonathani, asife.

Naye Yonathani akamwambia Daudi, Nenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la BWANA ya kwamba, BWANA atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.

Naye Sauli akamwapia kwa BWANA, akasema, Aishivyo BWANA, haitakupata adhabu yoyote kwa jambo hili.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo