Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.
Matendo 7:54 - Swahili Revised Union Version Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana, wakamsagia meno kwa hasira. Biblia Habari Njema - BHND Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana, wakamsagia meno kwa hasira. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana, wakamsagia meno kwa hasira. Neno: Bibilia Takatifu Wazee wa Baraza la Wayahudi waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. Neno: Maandiko Matakatifu Waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. BIBLIA KISWAHILI Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. |
Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.
Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.
Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Abrahamu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.