Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
Marko 9:32 - Swahili Revised Union Version Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo. Wakaogopa kumwuliza. Biblia Habari Njema - BHND Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo. Wakaogopa kumwuliza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo. Wakaogopa kumwuliza. Neno: Bibilia Takatifu Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake. BIBLIA KISWAHILI Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. |
Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huko kufufuka katika wafu maana yake nini?
Lakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile.
Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo.
Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nilisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?
Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye?