Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kusihi kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
Marko 9:29 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.” Biblia Habari Njema - BHND Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akawajibu, “Pepo aina hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba [na kufunga].” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawajibu, “Hali hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba na kufunga.” BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba. |
Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kusihi kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [
Alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.
katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.