Marko 8:18 - Swahili Revised Union Version Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki Biblia Habari Njema - BHND Je, mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki Neno: Bibilia Takatifu Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? Neno: Maandiko Matakatifu Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? BIBLIA KISWAHILI Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki? |
Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.
Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamuoni; mlio na masikio ila hamsikii.
Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.
Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.
lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi.
Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo.