Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Marko 4:12 - Swahili Revised Union Version

12 ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 ili, ‘Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 ili, ‘Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 ili, ‘Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 ili, “ ‘kuona waone lakini wasitambue, na kusikia wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka na kusamehewa!’”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 ili, “ ‘daima waone lakini wasitambue, daima wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.

Tazama sura Nakili




Marko 4:12
18 Marejeleo ya Msalaba  

Walete watu wasioona, japo wana macho, wasiosikia japo wana masikio.


Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.


Huenda nyumba ya Yuda watasikia mabaya yote niliyokusudia kuwatenda; wapate kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nami nikawasamehe uovu wao na dhambi yao.


Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamuoni; mlio na masikio ila hamsikii.


Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.


Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki?


Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.


Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;


lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi.


akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli;


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumtweza hadharani kwa dhahiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo