Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.
Marko 6:4 - Swahili Revised Union Version Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani mwake.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.” BIBLIA KISWAHILI Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. |
Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.
Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri.
Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe.
Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii anayekubaliwa katika nchi yake mwenyewe.
Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.