Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu.
Marko 4:40 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?” Biblia Habari Njema - BHND Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?” Neno: Bibilia Takatifu Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?” BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? |
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu.
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?
Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamna mikate?
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?