Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Marko 15:47 - Swahili Revised Union Version Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa. Biblia Habari Njema - BHND Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa. Neno: Bibilia Takatifu Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa. Neno: Maandiko Matakatifu Maria Magdalene na Maria mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa. BIBLIA KISWAHILI Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekwa. |
Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Na pale walikuwapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.
Na sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwemo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Naye akanunua sanda ya kitani, akamteremsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
Na sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.
Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa.