Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Marko 15:11 - Swahili Revised Union Version Lakini wakuu wa makuhani wakawachochea watu, kuwa afadhali awafungulie Baraba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba. Biblia Habari Njema - BHND Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba. Neno: Bibilia Takatifu Lakini viongozi wa makuhani wakachochea umati ule wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini viongozi wa makuhani wakauchochea ule umati wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake. BIBLIA KISWAHILI Lakini wakuu wa makuhani wakawachochea watu, kuwa afadhali awafungulie Baraba. |
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.
Pilato akajibu tena akawaambia, Basi nimtendeje huyu mnayemnena kuwa ni mfalme wa Wayahudi?
Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.