Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa BWANA, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya.
Marko 12:11 - Swahili Revised Union Version Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu.’” Biblia Habari Njema - BHND Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu.’” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu.’” Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu ndiye alitenda jambo hili, nalo ni la kushangaza machoni petu’?” Neno: Maandiko Matakatifu Mwenyezi Mungu ndiye alitenda jambo hili, nalo ni ajabu machoni petu’?” BIBLIA KISWAHILI Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? |
Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa BWANA, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya.
Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni la ajabu machoni petu?
ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.