Marko 11:32 - Swahili Revised Union Version Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu – waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.) Biblia Habari Njema - BHND Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.) Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu…’” (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.) Neno: Bibilia Takatifu Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu’ ” (waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yahya alikuwa nabii wa kweli); Neno: Maandiko Matakatifu Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’…” (Waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yahya alikuwa nabii wa kweli.) BIBLIA KISWAHILI Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu – waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi. |
Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini?
Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.
Nao wakataka kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.
Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.
Nao waandishi na wakuu wa makuhani walitaka kumkamata saa iyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao.
Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.
Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini yote aliyoyasema Yohana kuhusu habari zake huyu yalikuwa kweli.
Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.