Maombolezo 5:8 - Swahili Revised Union Version Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watumwa ndio wanaotutawala, wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao. Biblia Habari Njema - BHND Watumwa ndio wanaotutawala, wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watumwa ndio wanaotutawala, wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao. Neno: Bibilia Takatifu Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao. Neno: Maandiko Matakatifu Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao. BIBLIA KISWAHILI Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. |
Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?
Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu.
Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitamwokoa yeyote kutoka kwa mkono wao.