Maombolezo 5:22 - Swahili Revised Union Version Ingawa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Au, je, umetukataa kabisa? Je, umetukasirikia mno? Biblia Habari Njema - BHND Au, je, umetukataa kabisa? Je, umetukasirikia mno? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Au, je, umetukataa kabisa? Je, umetukasirikia mno? Neno: Bibilia Takatifu isipokuwa uwe umetukataa kabisa na umetukasirikia pasipo kipimo. Neno: Maandiko Matakatifu isipokuwa uwe umetukataa kabisa na umetukasirikia pasipo kipimo. BIBLIA KISWAHILI Ingawa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu. |
Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.
Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?
Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!
Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana BWANA amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.
Katika uchafu wako mna uasherati, kwa maana nimekusafisha, ila wewe hukusafika; hutasafishwa tena uchafu wako ukutoke, hadi nitakapokuwa nimeituliza hasira yangu kwako.
Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.
Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.