Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 64:9 - Swahili Revised Union Version

9 Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu, usiukumbuke uovu wetu daima! Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu, usiukumbuke uovu wetu daima! Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu, usiukumbuke uovu wetu daima! Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Ee Mwenyezi Mungu, usikasirike kupita kiasi, usizikumbuke dhambi zetu milele. Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, kwa kuwa sisi sote tu watu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Ee bwana, usikasirike kupita kiasi, usizikumbuke dhambi zetu milele. Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, kwa kuwa sisi sote tu watu wako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.

Tazama sura Nakili




Isaya 64:9
27 Marejeleo ya Msalaba  

Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako.


Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.


BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.


Na sisi tulio watu wako, Na kondoo za malisho yako, Tutakushukuru milele; Tutazisimulia sifa zako kizazi hadi kizazi.


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.


Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nilikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.


Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.


Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.


Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.


Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.


Nenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema BWANA; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema BWANA, sitashika hasira hata milele.


Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! BWANA hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?


Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA Kama katika sikukuu.


Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.


Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi?


Ingawa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.


Wala hautakuwa tena tegemeo la nyumba ya Israeli, kufanya maovu yakumbukwe, watakapogeuka kuangalia nyuma yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.


Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.


Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.


Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.


Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.


Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo